Swali: Je, mtu anaweza kusema kuwa fisi ni mnyamamkali aliyebaguliwa katika wanaofaa kuliwa?

Jibu: Ndio, fisi amevuliwa. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu fisi. Akasema: ”Ni kitoweo.”[1]

Yule asiyetaka kula nyama ya fisi hakulazimishwa. Uamuzi uko kwake.

[1] Abu Daawuud (3801). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (3801).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (41)
  • Imechapishwa: 12/10/2023