46. Kuna vita gani vingine vilitokea mwaka wa 3?

Swali 46: Kuna vita gani vingine vilitokea mwaka wa tatu?

Jibu: Vita vya Dhuu Amar ambavo viliendelea mwezi wote wa Safar.

Vita vya Furuu´ mwishoni mwa mwezi wa Rabiy´ al-Awwal.

Vita vya Banuu Qaynaqaa´. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowashinda kiongozi wa wanafiki Ibn Saluul akapinga na kuwaachia huru.

Vita vya Uhud katikati ya Shawwaal. Wakati wa mnasaba wa vita hivyo kukawekwa Shari´ah ya kuacha kuwaswalia mashahidi na badala yake kuzikwa wakiwa na nguo na damu zao. Kukaruhusiwa kumzika zaidi ya mmoja ndani ya kaburi moja kutokana na dharurah pamoja na kuwazika pale walipouliwa.

Vita vya Hamraa´-ul-Asad. Ndipo kukateremshwa juu ya hilo:

وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ 

”Na pale uliporauka ukaacha familia yako ili uwapangie waumini kwenye vituo kwa ajili ya vita; na Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa kila kitu.”[1]

mpaka:

مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَجْتَبِي مِن رُّسُلِهِ مَن يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ 

”Haiwi kwa Allaah kuwaacha waumini katika hali mliyomo mpaka ampambanue mbaya na mwema. Na haiwi kwa Allaah akufichukulieni ya ghaibu, lakini Allaah humteua katika Mitume Yake amtakaye. Basi mwaminini Allaah na Mtume Wake; na mkiamini na mkamcha Allaah basi mtapata ujira mkuu kabisa.”[2]

[1] 3:121

[2] 3:179

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 110-111
  • Imechapishwa: 12/10/2023