Swali: Kuna kigezo kipi cha damu inayotoka mwilini inayoharibu swawm? Inaharibu swawm vipi?

Jibu: Damu inayoharibu swawm ni ile damu inayotoka kwa kuumikwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa chuku.”[1]

Kunatumiwa kipimo juu ya chuku kile chenye maana yake katika yale yanayofanywa na mtu kwa kutaka kwake mwenyewe ambapo akatokwa na damu nyingi inayodhoofisha mwili. Damu kama hiyo inaharibu swawm kama kuumikwa. Shari´ah ya Uislamu haitofautishi kati ya vitu viwili vinavyofanana kama ambavyo haikusanyi kati ya vitu viwili vinavyofanana.

Kuhusu damu inayomtoka mtu pasi na kukusudia, kama mfano wa damu ya puani, jeraha mwilini kutokana na kisu wakati wa kukata nyama, kukanyaga kioo na mfano wa hayo, hayaharibu swawm ijapo mtu atatokwa na damu nyingi. Vivyo hivyo akitokwa na damu kidogo isiyomdhoofisha kama inavyodhoofisha chuku, kama ile damu inayochukuliwa kwa ajili ya kipimo, haiharibu swawm.

[1] Ahmad (8550) na at-Tirmidhiy (774).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/11871/ضابط-الدم-الخارج-من-الجسد-المفسد-للصوم
  • Imechapishwa: 30/03/2023