Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن أم المؤمنين أم عبد الله عائشة رضي الله عنها قالت: قال رسول الله صلي الله عليه وسلم: ((يغزو جيش الكعبة فإذا كانوا ببيداء من الأرض يخسف بأولهم وآخرهم)) قالت: يا رسول الله، كيف تخسف بأولهم وآخرهم وفيهم اسوافهم، ومن ليس منهم؟ قال: ((يخسف بأولهم وآخرهم ثم يبعثون على نياتهم)) (متفق عليه) هذا لفظ البخاري

02 – Mama wa waumini, Umm ‘Abdillaah, ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa), ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Jeshi litataka kuivamia Ka’bah. Litakapofika katika ardhi ya jangwa, basi watadidimizwa wa mwanzo na wa mwisho wao.” Nikauliza: “Ee Mtume wa Allaah, vipi wote wa mwanzo na wa mwisho wao watadidimizwa na miongoni mwao kuna raia wa kawaida na hawakuwa miongoni mwao?” Akajibu: “Wote wa mwanzo na wa mwisho wao watadidimizwa kisha watafufuliwa kutegeme nia zao.”

Kuna maafikiano juu yake na tamko ni la al-Bukhaariy.

Katika Hadiyth hii kuna mazingatio juu ya kwamba yule anayeshirikiana na watu wa batili, watu wa dhuluma na uadui basi atashirikiana nao katika adhabu. Mwema na muovu. Kunapoteremshwa adhabu inampata mwema na muovu, muumini na kafiri, mwenye kuswali na mwenye kufanya kiburi. Adhabu haimwachi yeyote. Siku ya Qiyaamah kila mmoja atafufuliwa juu ya nia yake. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَاتَّقُوا فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُوا مِنكُمْ خَاصَّةً ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ

“Na ogopeni fitina ambayo haitowasibu pekee wale waliodhulumu [nafsi zao] miongoni mwenu na tambueni kwamba Allaah ni mkali wa kuadhibu.” (08:25)

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/30)
  • Imechapishwa: 16/01/2023