Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

وعن عائشة – رضي الله عنها- قالت: قال النبي صلي الله عليه وسلم ((لا هجرة بعد الفتح ولكن جهاد ونبة وإذا استفرتم فانفروا)) متفق عليه

03 – ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna kuhajiri isipokuwa baada Ufunguzi [wa mji wa Makkah] na mtakapoambiwa tokeni [kwenda vitani] basi tokeni.”

Bi maana pale ambapo mtawala atawaambia tokeni mwende katika Jihaad katika njia ya Allaah basi tokeni mwende kwa njia ya uwajibu. Katika hali hiyo Jihaad itakuwa ni faradhi kwa kila mtu. Watu watapoambiwa kutoka kwenda katika Jihaad basi ni wajibu kwao kutoka na nyuma asibaki yeyote isipokuwa yule aliyepewa udhuru na Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ 

“Enyi mlioamini! Mtapokutana na wale waliokufuru vitani, msiwageuzie migongo [kukimbia]. Na yeyote yule atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo [atakuwa mkosa] isipokuwa akigeuka kwa kufanya mbinu za kupigana au [amegeuka] kwa kujiunga na kikosi [kingine cha waislamu. Vinginevyo], basi amestahiki ghadhabu ya Allaah na makazi yake ni [Moto wa] Jahannam – na ni pabaya palioje mahali pa kuishia!”  (08:15-16)

Hii ni hali moja wapo ambapo Jihaad inakuwa faradhi kwa kila mtu.

2 – Hali ya pili ni pale ambapo adui anapovamia mji. Anapokuja adui mpaka akafika katika mji na kuuvamia, basi Jihaad inakuwa ni faradhi kwa kila mtu. Ni wajibu kwa kila mtu kupambana. Hata kwa mwanamke na mzee mwenye uwezo katika hali hii. Kwa sababu hivi ni vita vya kujihami. Kuna tofauti kati ya Jihaadi ya kujihami na Jihaad ya kushambulia. Katika hali hii ni wajibu kwa watu wote kutoka ili waweze kuuhami mji wao.

3 – Hali ya tatu ni pale wanapofika katika safu na kusimama safu mbili: safu ya makafiri na ya waislamu. Katika hali hii Jihaad inakuwa ni faradhi kwa kila mtu. Haijuzu kwa yeyote kuondoka. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا زَحْفًا فَلَا تُوَلُّوهُمُ الْأَدْبَارَ وَمَن يُوَلِّهِمْ يَوْمَئِذٍ دُبُرَهُ إِلَّا مُتَحَرِّفًا لِّقِتَالٍ أَوْ مُتَحَيِّزًا إِلَىٰ فِئَةٍ فَقَدْ بَاءَ بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ 

“Enyi mlioamini! Mtapokutana na wale waliokufuru vitani, msiwageuzie migongo [kukimbia]. Na yeyote yule atakayewageuzia mgongo wake siku hiyo [atakuwa mkosa] isipokuwa akigeuka kwa kufanya mbinu za kupigana au [amegeuka] kwa kujiunga na kikosi [kingine cha waislamu. Vinginevyo], basi amestahiki ghadhabu ya Allaah na makazi yake ni [Moto wa] Jahannam – na ni pabaya palioje mahali pa kuishia!”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya kukimbia siku ya vita ni katika madhambi saba yenye kuangamiza.

4 – Hali ya nne ni pale ambapo mtu atapohitajika. Kwa mfano silaha hakuna yeyote anayejua kuitumia isipokuwa mtu fulani na hivyo watu wakawa ni wenye kumuhitaji mtu huyu ili atumie silaha hii ambayo kwa mfano ni mpya. Katika hali hii ni wajibu juu yake kupambana hata kama katika Jihaad hakuteuliwa. Hili ni kwa sababu anahitajika juu ya hilo. Katika hali hizi nne Jihaad inakuwa ni faradhi kwa kila mtu. Mbali na hali hizi Jihaad inakuwa ni faradhi kwa baadhi ya watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/32-33)
  • Imechapishwa: 16/01/2023