Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Kuonekana ni haki kwa watu wataokuwa Peponi – pasi na kumzunguka wala kulifanyia namna.”

Watu hawawezi kumzunguka Allaah (´Azza wa Jall). Watamuona pasi na kumzunguka. Allaah ni mtukufu na hawezi kuzungukwa. Amesema (Subhaanah):

يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Anajua yale yaliyoko mbele yao na yale yaliyoko nyuma yao na hawawezi kumzunguka kwa kumtambua.”[1]

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”[2]

Bi maana hayamzunguki. Maana yake si kwamba hayawezi kumtazama. Kuzunguka ni kitu na kuonekana ni kitu kingine. Allaah hakusema kuwa macho hayamuoni, alichosema ni:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”

Kukizunguka kitu ni kitu kimoja na kuonekana ni kitu kingine. Macho  yatamuona, lakini pasi na kumzunguka. Hapa wanaraddiwa wale waliojengea hoja Aayah hii katika kupinga Kuonekana na wakasema kuwa ni jambo lisilowezekana kwa sababu Allaah amesema:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارَ

“Macho hayamzunguki.”

Hawafahamu maana. Aayah inasema kuwa macho hayawezi kumzunguka, na si kwamba hayamuoni.

[1] 20:110

[2] 6:103

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 77-78
  • Imechapishwa: 16/01/2023