Hakuna waliopinga Kuonekana isipokuwa tu Ahl-ul-Bid´ah kama mfano wa Jahmiyyah na Mu´tazilah. Wao wanaona kuwa kuthibtisha kuonekana kunapelekea Allaah kuwepo upande fulani, ilihali wao wanaona kuwa Allaah hayuko upande wowote. Kwa mujibu wao wanaona kuwa Allaah hayuko ndani ya ulimwengu wala nje yake, hayuko juu yake wala chini yake, wala kuliani mwake wala kushotoni mwake. Kwa msemo mwingine Allaah hayuko katika upande wowote. Hiyo maana yake ni kwamba Allaah hayupo kabisa. Allaah ametakasika kutokamana na wanayoyasema! Kwa hiyo wamepinga kuonekana kwa sababu ya rai hii batili.

Kuhusu Ashaa´irah wao waliona kuwa hawawezi kupinga dalili kuhusu kuonekana kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah. Hivyo wakathibitisha Kuonekana, lakini wakasema bila ya kuwa upande wowote. Huu ni mkanganyiko wa ajabu. Hakuna kitu kinachoonekana isipokuwa kinakuwa upande fulani. Kwa ajili hiyo Mu´tazilah wakawaraddi na kuwatuhumu kuwa ni kitu kisichowezekana kabisa. Ahl-us-Sunnah wao wanasema kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ataonekana akiwa upande wa juu, juu ya watu.

Ikiwa kupinga kwao wanakusudia upande ulioumbwa, ni kweli kwamba Allaah hayuko katika upande huo; hawezi kukita ndani ya viumbe Vyake. Ikiwa upande wanakusudia uwepo wa Allaah juu ya viumbe, hicho ni kitu kimethibiti kwa Allaah. Allaah (Ta´ala) yuko juu, juu ya mbingu. Isitoshe neno upande halikupokelewa kuthibitishwa wala kupingwa kwake ndani ya Qur-aan. Hata hivyo kunasemwa juu yake kutokana na upambanuzi uliotangulia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 16/01/2023