Khatari ya kusimama kabla ya Tasliym ya pili ya imamu

Swali: Maamuma waliojiunga na mkusanyiko kwa kuchelewa wanaweza kusimama moja kwa moja baada ya Tasliym ya kwanza ya imamu?

Jibu: Wanachuoni wanasema mwenye kusimama baada ya Tasliym ya kwanza basi swalah yake inabadilika kutoka katika swalah ya faradhi kwenda katika swalah ya Sunnah. Mwenye kusimama kabla ya Tasliym ya pili swalah yake inabadilika kwenda katika swalah ya Sunnah. Kwa hivyo ni lazima aswali swalah ya faradhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020