Kuwepo neno “HALAAL” (حلال) kwenye paketi kunatosheleza?

Swali: Kuwepo kwa neno “HALAAL” (حلال) kwenye paketi ya nyama kunaondosha utata kwamba haikuchinjwa kwa njia isiyokuwa ya Kishari´ah?

Jibu: Hapana. Kuna uwezekano paketi hii ikawa ni ya nyama nyingine. Vilevile huenda wanataka kuwahadaa watu ndio maana wakaziweka ndani ya paketi hii. Jambo hilo halifanyi kuwa zimechinjwa kwa njia ya Kishari´ah maadamu hakuna cheti au muhuri wenye kuaminika juu yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020