Kazi kwenye benki ikiwa nimekosa kazi nyingine

Swali: Mimi nafanya kazi katika benki ya Uingereza ya Saudia kwa muda wa miaka kumi na benki hiyo inatoa mikopo ya ribaa. Je, kazi yangu katika benki ya ribaa ni haramu pamoja na kuzingatia kuwa nimetafuta kazi nyingine sikupata?

Jibu: Ndio. Haijuzu kufanya kazi mahali hapo. Muda wa kuwa ni benki ya ribaa usifanye kazi mahali hapo. Allaah atakuruzuku kazi nyingine bora kuliko hiyo. Allaah (Subhaanah) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yule anayemcha Allaah, basi humjaalia njia [ya kutokea] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.”[1]

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا

“Na yeyote yule anayemcha Allaah, basi atamjaalia wepesi katika jambo lake.”[2]

Ni lazima kwako kujiweka mbali na ribaa hii na kutubu kutokana na yaliyotangulia.

[1] 65:02-03

[2] 65:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22132/هل-يجوز-العمل-في-البنوك-الربوية
  • Imechapishwa: 31/10/2022