Kipi bora kutafuta mali nyingi au kinyume chake?

Swali: Ni kipi bora mtu amwombe Allaah ampe kichache cha dunia au amzidishie mali?

Jibu: Akiwa anataka kutendea kazi kumtii Allaah na kuwanufaisha waislamu basi analazimika kufanya sababu muda wa kuwa shughuli hizo hazimshughulishi kutokamana na Aakhirah. Afanye kazi ili baadaye anawanufaishe watu kama walivofanya Maswahabah akiwemo Abu Bakr, ´Umar na ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf (Radhiya Allaahu ´anhum). Walijitolea katika njia ya Allaah na wakafanya vizuri. Kwa sharti dunia hiyo isimshughulishe kutokamana na Aakhirah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22180/هل-طلب-التزود-من-المال-افضل-ام-التقلل
  • Imechapishwa: 31/10/2022