Katika hali hii mali si milki ya mgonjwa tena

Mtu ambaye ana ugonjwa ambao kunakhofiwa juu yake mauti haifai kutoa swadaqah zaidi ya theluthi. Kwa sababu mali yake [katika hali hii] inakuwa ni yenye kufungamana na haki ya wengine ambao ni warithi. Ama kuhusu mtu ambaye ana afya njema na hana maradhi au ana maradhi madogo ambayo yakukhofiwi juu yake mauti, ana khiyari ya kutoa swadaqah kwa kiasi anachotaka. Ni mamoja ikiwa ni theluthi, nusu, theluthi mbili au mali yake yote. Hakuna ubaya juu ya hilo. Lakini hata hivyo haitakikani kwake kutoa mali yake yote isipokuwa yuko na kitu [anachomiliki] ambacho anajua kuwa atajitosheleza nacho kwa kuwaomba watu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/43)
  • Imechapishwa: 22/01/2023