Katika hali hii itafaa kukidhi haja kwa kuelekea Qiblah

Swali: Hadiyth ya Ibn ´Umar wakati alipomuona Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyumbani kwa Hafswah akikidhi haja yake hali ya kuelekea Qiblah inafasiriwa kuwa ni jambo maalum kwake?

Jibu: Hapana, si maalum kwake. Hadiyth inafahamisha kuwa sio haramu kukidhi haja kwa kuelekea Qiblah ikiwa ni ndani ya nyumba. Hapana vibaya akielekea Ka´bah au akiipa mgongo muda wa kuwa yuko ndani ya nyumba. Kilichoharamishwa [ni kuielekea Ka´bah] mtu akiwa sehemu ya wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23042/حكم-قضاء-الحاجة-مستدبر-الكعبة-في-البنيان
  • Imechapishwa: 21/10/2023