Baada ya kumalizika swalah ya Fajr Adhkaar au kusoma Qur-aan?

Swali: Je, bora ni kusoma Adhkaar zilizopokelewa za asubuhi au kusoma Qur-aan?

Jibu: Bora baada ya kutoa salamu ni yale aliyobainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndio Sunnah yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Swalah inapomalizika basi imamu na maamuma waseme:

أستغفر الله

“Allaah nisamehe.”

Mara tatu.

واللهم أنت السلام ومنك السلام تباركت يا ذا الجلال والإكرام

“Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam, amani inatoka Kwako, umebarikika, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”

Kisha baada ya hapo wasome zile Adhkaar zilizowekwa katika Shari´ah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23041/هل-الافضل-بعد-الفجر-الذكر-ام-التلاوة
  • Imechapishwa: 21/10/2023