Subha inafaa, lakini bora zaidi ni kwa vidole

Swali: Kumdhukuru Allaah kwa Subha?

Jibu: Hapana vibaya. Hata hivyo bora ni kufanya hivo kwa vidole. Lakini ni sawa pia akimtaja Allaah kwa kokoto, Subha, mbegu na vyenginevyo. Yamefanywa na baadhi ya Salaf na baadhi ya Maswahabah wa kike. Hata hivyo bora zaidi ni kwa vidole. Ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kuhesabu kwa vidole ndio bora. 

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23044/ما-حكم-التسبيح-بالمسبحة
  • Imechapishwa: 21/10/2023