Matajiri wenye kushukuru au masikini wenye kusubiri?

Swali: Hadiyth ya Abu Hurayrah inajulisha kuwa matajiri ni bora kuliko mafukara?

Jibu: Wamefanya matendo ya mafukara na wakazidisha juu yao kwa kutoa swadaqah kwa mujibu wa matendo yao. Kila ambavo yatazidi matendo mema ndivo unavyozidi ubora. Tajiri mwenye kushukuru ni bora kuliko fakiri kwenye kusubiri, kwa sababu tajiri huyu yuko na uwezo wa kufanya maasi, lakini Allaah akamlinda na akamtumia katika mambo ya utiifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23046/من-الافضل-الغني-الشاكر-ام-الفقير-الصابر
  • Imechapishwa: 21/10/2023