55. Ni Aayah zipi zilizoteremshwa zinazofuta mwaka wa 6?

Swali 55: Ni Aayah zipi zilizoteremshwa zinazofuta kuhusiana na jambo hilo?

Jibu: Kulishushwa Aayah za mtihani kuhusu wanawake wanaohajiri. Wakati imani yao inapojaribiwa na kuthibitishwa, basi haifai kuwarudisha kwa washirikina. Kwa sababu wanawake hao hawahalaliki kwa wanaume wao wala wanaume hao hawahalaliki kwa wanawake hao. Aidha Quraysh wakaondoa sharti lao kwamba waislamu Wahamiaji warudishwe Makkah. Sababu ilikuwa kwamba waislamu waliorudi waliungana na wengine njiani na wanawakatia njia yao.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 118
  • Imechapishwa: 21/10/2023