Katika hali hii inafaa kuwatii wazazi katika kumtaliki mke

Swali: Mama akimuamrisha mtoto wake kumtaliki mke wake. Je, ni wajibu kumtaliki na asipofanya hivo anakuwa ni mwenye kumuasi?

Jibu: Hapana. Mmoja katika wazazi akikuamrisha kumtaliki mke wake pasi na sababu ya Kishari´ah, sio lazima kufanya hivo. Ama ikiwa ni kwa sababu ya Kishari´ah kwa kuwa ana mapungufu katika dini yake, anawaudhi wazazi wake au mmoja katika wazazi, amtii katika hilo. Ama ikiwa ni pasi na sababu, bali ni chuki tu binafsi, sio lazima kumtaliki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (73) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-21.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020