Maamuma kumfuata imamu katika Rak´ah aliyozidisha

Swali: Imamu alituswalisha ´Ishaa Rak´ah tano na tukamzindua lakini hakurudi. Mimi nikawa nimekaa na sikumfuata na baadae nikatoa salamu pamoja naye. Hata hivyo maamuma wengine walimfuata. Ni ipi hukumu ya swalah yangu na ya kwao?

Jibu: Swalah yako ni sahihi. Maadamu una uhakika kuwa amezidisha, haijuzu kwako kumfuata. Kukaa kwako ni wajibu. Unatakiwa kukaa na ima utoe salamu kivyako au ungoje na kutoa salamu pamoja nao.

Kuhusu maamuma wengine waliomfuata, ikiwa ni wajinga, swalah zao ni sahihi na wanapewa udhuru kwa ujinga. Ama ikiwa ni mtu anayejua, swalah yake inabatilika. Ikiwa anajua kuwa imamu amezidisha na anajua kuwa haijuzu kumfuata imamu [katika hali hii], swalah yake inabatilika.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (73) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-21.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020