Dawa inatoka kwa Allaah na si kwenye kisomo

Swali: Wakati wa kutumia Ruqyah ya Qur-aan na du´aa za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa ni pamoja na zaituni na maji ya zamzam, tuamini kuwa dawa iko kwenye maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) au ni sababu tu na dawa inatoka kwa Allaah?

Jibu: Hili halina shaka. Ruqyah ni sababu. Dawa inatoka kwa Allaah (´Azza wa Jall). Haijuzu kutegemea Ruqyah. Mtegemewaji ni Allaah. Hili linahusu sababu zote. Haijuzu kuzitegemea. Mtegemewaji ni Allaah (Jalla wa ´Alaa).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (73) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-10-21.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020