Katika dini mtazame aliye juu yako – katika dunia mtazame aliye chini yako

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا تَمُدَّنَّ عَيْنَيْكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعْنَا بِهِ أَزْوَاجًا مِّنْهُمْ زَهْرَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا لِنَفْتِنَهُمْ فِيهِ ۚ وَرِزْقُ رَبِّكَ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ

“Na wala usikodolee macho yako kwa yale Tuliyowastareheshea baadhi ya watu miongoni mwao, kwani hayo ni mapambo ya uhai wa dunia tu ili tuwafitinishe kwavyo. Na riziki ya Mola wako ni bora zaidi na ni yenye kubakia.” (20:131)

Usiikodolee macho dunia, ukataka kuwapokonya wenye nayo na ukatamani kupata mfano wa walionayo.

Kuhusu dunia mtazame yule aliye chini yako. Kuhusu dini mtazame yule aliye juu yako ili uweze kushindana naye. Dunia mtazame yule aliye chini yako ili upate kuona neema za Allaah juu yako. Kuna watu wako chini katika maisha haya ya dunia, sawa inapokuja katika mali, siha, afya na nyumba. Utapowatazama watu hawa [na ukaona tofauti kubwa kati yako wewe na wao], basi zikumbuke neema za Allaah juu yako na uziadhimishe na kuzishukuru.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaaswid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/427)
  • Imechapishwa: 26/08/2020