Katika ardhi ya vipofu mwenye chongo huwa mfalme

Baada ya hapo msomaji akaanza kusoma maneno ya yule anayedaiwa kuwa eti ni Shaykh al-Albaaniy. Yule anayedaiwa eti ni Shaykh. Namaanisha kweli. Kwa sababu mimi naamini kabisa ndani ya moyo wangu ya kwamba mfano wangu hii leo naingia ndani ya ile methali ya aliyesema:

”Katika ardhi ya vipofu mwenye chongo huwa mfalme.”[1]

Msichukulie vibaya. Nina haki ya kujizungumzia mwenyewe, lakini sina haki ya kuwazungumzia wengine, ingawa haya yanaweza kuwagusa wengine. Kwa ajili hiyo nasema:

”Katika ardhi ya vipofu mwenye chongo huwa mfalme.”

Mimi ni mwenye chongo na katika ardhi kuna vipofu. Ukweli wa mambo haya ndio ambayo namwabudu Allaah kwayo na kwamba ulimwengu umekosa wanachuoni ambao sisi tunatambua hadhi zao na kuwatukuza kama mfano wa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Hii leo tunatajwa sambamba nao, lakini wapi na wapi… Hapa kunanasibiana kutaja nathari inayosema:

Vipi udongo unaweza kulinganishwa na nyota?

Vipi Mu´aawiyah anaweza kulinganishwa na ´Aliy?

Mu´aawiyah pia ni Swahabah, lakini kuna tofauti kubwa kati ya hao watu wawili. Mimi ni mwanafunzi tu. Lakini ni vipi sisi tunaweza kulinganishwa na wanachuoni hao? Ndio maana narudi kusema:

”Katika ardhi ya vipofu mwenye chongo huwa mfalme.”

[1] Yamesemwa na Niccolò Machiavelli (afk. 1527).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (940)
  • Imechapishwa: 12/12/2020