Swali: Nilioa nami nilikuwa bado mdogo, na baada ya kuoa kwa takriban miezi kama mitatu nikwamwambia mke wangu mara nyingi: “Mimi sikutaki!”. Waambie wazazi wako kuwa mimi sikutaki”, pamoja na kuwa ni mke mwema. Na sasa sijui maneno niliyomwambia mke wangu huchukuliwa nimemtaliki au hapana? Kwa kuwa sikukusudia kumtaliki kwa kumwambia hivyo. Na ikiwa kama nimemtaliki, je nifunge nae ndoa upya kwa mara ya pili?
Jibu: Maneno haya haiwi talaka, uliyasema bila ya kukusudia hivyo, haiwi talaka. Maadamu hakunuwia talaka, si talaka. Bado ni mke wake.
Swali: Je, ana kafara yoyote kwa hilo?
Jibu: Hana juu yake kitu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.alharamain.gov.sa/index.cfm?do=cms.scholarallsubjects&schid=8177
- Imechapishwa: 01/02/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related

Mambo ya talaka lazima yadhibitiwe na yasijiliwe
https://www.youtube.com/watch?v=_TJw-eB1zto Swali: Nilimtaliki mke wangu nami wakati huyo nilikuwa na maradhi ya sukari na mengine na nilikuwa katika hali ya khasira nyingi. Na sijui ni mara ngapi nimemtaliki mke huyu kama ni mara moja au zaidi. Mke wangu anasema kuwa nimemtaliki mara tatu na mimi sujui ni mara ngapi. Isipokuwa…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"

Vipi tuseme katoa talaka moja naye anasema katoa tatu
https://www.youtube.com/watch?v=pu-AMDRIPxk Swali: Nilimtaliki mke wangu nami wakati huyo nilikuwa na maradhi ya sukari na mengine na nilikuwa katika hali ya khasira nyingi. Na sijui ni mara ngapi nimemtaliki mke huyu kama ni mara moja au zaidi. Mke wangu anasema kuwa nimemtaliki mara tatu na mimi sujui ni mara ngapi. Isipokuwa…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"

Baada ya talaka tatu hakuna kumrudi mke
https://www.youtube.com/watch?v=anUqqh_6QxY Swali: Nilimtaliki mke wangu mara tatu. Mara ya kwanza ilikuwa wakati wa Maghrib aliponambia maneno yaliyonikasirikisha nikawa nimemtaliki na (baadae) nikamrejea na kumrudisha nyumbani kwa kuwa ni mama wa watoto wangu wawili. Na baada ya siku kukatokea baina yetu magomvi, nikawa nimemtaliki. Akaingia kwangu na kuniomba nimrudi kwa ajili…
In "Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz"