Kabila kumsimamishia mtu adhabu katika nchi isiyohukumu kwa Shari´ah

Swali: Kuna muulizaji nje ya nchi hii – Saudi Arabia – anasema kuwa katika mji wao kuna mtu amewaua watu wawili. Mtawala katika mji huo hana nguvu wala mamlaka ya kusimamisha adhabu ya Kishari´ah na kisasi. Je, kabila linaweza kumsimamishia adhabu ya Kishari´ah sawa ikiwa ni kabila lake au makabila ya watu wawili?

Jibu: Hakuna anayesimamisha kisasi na kusimamisha huduud isipokuwa mtawala ili kusitoee vurugu na mauaji baina ya watu. Hakuna anayefanya hili isipokuwa mtawala.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (03) Sharh Zaad-il-Ma´aad (74) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14131
  • Imechapishwa: 17/11/2014