Elimu ya kwanza mtoto hupata, ni elimu ya wazazi wake na khaswa mama. Mama ana nafasi kubwa katika kuongoza na kutunza vizazi. Mapote potevu ya Kiislamu hayapuuzi hili. Kwa ajili hii ndio maana wameshikilia mafungamano na kufungua mashule na vyuo vikuu na shule za Qur-aan khaswa kwa wanawake. Makundi haya yanaeneza nadhariya zao kupitia mikanda inayochezeshwa wanafunzi wa makundi ambao kwa upande wao wanaitwa “wanachuoni”. Kadhalika, wanagawa vijitabu na vipeperushi. Huenda malengo yao yasitoke kwa mara moja. Hata hivyo, hili linapelekea kwa wanawake kuanza kutegemea wanafunzi hawa na kuwachukulia kama marejeleo ya kielimu. Halafu wanawaingiza fikira hizo na mielekeo kama wanavyopenda.

Kutokana na hili, tunasema yale yale tuliyosema kuhusu vijana na kwamba tunakata njia kwa makundi haya kwa kuwafanya wanawake waweze kurejea kwa wanachuoni wakubwa, kusambaza mikanda na Fataawaa zao, kutahadharisha makundi potevu, kufichukua kampeni na malengo yao na kuwalea watoto wao kutokana na mfumo wa Salaf na kupenda elimu na wanachuoni[1].

[1] ‘Allaamah ‘Abdul-‘Aziyz bin ‘Abdillaah Aalish-Shaykh (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Kitabu cha muheshimiwa Shaykh ‘Abdus-Salaam bin ‘Abdillaah as-Sulaymaan ‘Silat-ul-Ghuluww Fiyt-Takfiyr bil-Jariymah” kwa hakika ni kazi ya shahaadah ya udaktari. Nilikuwa pamoja na ndugu yangu, muheshimiwa Shaykh Swaalih al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah), mmoja katika wale waliojadiliana naye. Amefikia shahaadah yake ya pili na amependekeza kuichapisha kazi hii. Hii ni kazi ya umakini, ilio na thamani na yenye manufaa katika tawi lake. “(Dibaji ya ” Silat-ul-Ghuluww Fiyt-Takfiyr bil-Jariymah”, uk. 3)

‘Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Kitabu cha Shaykh ‘Abdus-Salaam bin ‘Abdillaah as-Sulaymaan ‘Silat-ul-Ghuluww Fiyt-Takfiyr bil-Jariymah” ni kitabu chenye manufaa ambacho kinahitajika leo wakati tatizo hili, yaani. Takfiyr kwa yule asiyeistahiki, limeenea ili kusaidia kutatua jambo hili na kulitahadharisha. Hivyo, ni sawa kusambaza na kugawa kitabu hiki. “(Dibaji ya “Silat-ul-Ghuluww Fiyt-Takfiyr bil-Jariymah”, uk. 4).

  • Mhusika: Shaykh ‘Abdus-Salaam bin ‘Abdillaah as-Sulaymaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silat-ul-Ghuluww fiyt-Takfiyr bil-Jariymah , uk. 361-362
  • Imechapishwa: 23/04/2015