Allaah (´Azza wa Jall) Amesema:

“Na katika watu yupo mwenye kukuvutia kauli yake katika uhai wa dunia na humshuhudisha Allaah kwa yale yaliyomo katika moyo wake na hali yeye ndiye khasimu mbaya zaidi. Na anapotawala hujitahidi (kufanya akitakacho) katika ardhi ili afisidi humo na aangamize mimea na vizazi. Na Allaah Hapendi ufisadi. Na anapoambiwa: “Muogope Allaah!” Hupandwa na mori kwa (kutenda) dhambi. Basi (Moto wa) Jahannam unamtosheleza na ni pabaya palioje mahali pa kupumzika.” (02:204-206)

Allaah ni Mkubwa! Ni uzuri ulioje Aayah zinavyowagusa Khawaarij wa leo ambao wanaeneza ufisadi katika ardhi? Wanafungua njia ya hujuma na [wana] njaa kwa ajili hilo. Wanasema kuwa ni Jihaad. Uhakika wa mambo ni kwamba ni katika ufisadi mkubwa, umwagaji wa damu, machafuko, uharibifu wa mali na kuenea khofu kwa watu wasio na hatia. Huu ni ugaidi.

Hakuna shaka yoyote kwamba mimi na wengine tunaonelea kuwa watu hawa watapata mwisho mbaya kwa Allaah na matumaini yao juu ya uokovu yako mbali kabisa. Kwa sababu wameenda kinyume na maandiko ya Shari´ah na nasaha za wenye busara.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Muhabbar, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 23/04/2015