Hakuna shaka yoyote kwamba matendo ya kipote hichi potevu ni haramu na yamekatazwa kila mahala. Damu ya Waislamu ni haramu kuimwaga kila mahala. Hata hivyo ni khatari zaidi Makkah na al-Madiynah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameitakasa al-Madiynah al-Madiynah kama jinsi Ibraahiym alivyoitakasa Makkah. Ikiwa katika utufu wa Makkah ni haramu kukata miti yake, basi ni haramu zaidi kumagwa damu.

Hakika matendo ya kigaidi ya yule mpotevu lengo la kwanza kabisa ni uhai uliotakaswa ambao haijuzu kuukosesha amani. Miongoni mwa hao ni Waislamu na makafiri ambao wameahidiwa amani.

Uharamu wa kuleta hujuma na Bid´ah al-Madiynah yako wazi kabisa na yanajulikana kutokana katika mapokezi sahihi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kila mtu anajua Hadiyth ya laana ya Allaah impate yule mwenye kuzusha Bid´ah na kumlinda mtu wa Bid´ah al-Madiynah. Laana hii inampata kila mwenye kushiriki katika Bid´ah ambayo laana hii inapelekea. Inawapa wale wenye kupanga, wenye kufanya na wengine. Kadhalika inawapata wale wenye kuwalinda, kuwanyamazia na kuacha kuwajulisha wanaume wanaochunga usalama.

Katika darsa zetu katika Msikiti mtukufu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tunawatahadharisha vijana na fikira za pote hili na matokeo yake yenye kukatazwa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Gazeti ”al-Madiynah”, uk. 4
  • Imechapishwa: 23/04/2015