Jimaa ya wanandoa wasafiri waliofika katika mji wao

Swali: Mwanaume alikuwa yeye na mke wake wamesafiri mchana wa Ramadhaan kisha akarudi katika mji wake na kujizuia. Baada ya hapo mwanaume akamjamii mke wake. Je, analazimika kutoa kafara?

Ibn Baaz: Usiku au mchana?

Muulizaji: Mchana.

Jibu: Analazimika kutoa kafara. Anapofika katika mji wake analazimika yeye mwanaume na mwanamke kujizuia. Akimjamii ina maana amemjaami ndani ya Ramadhaan na katika utukufu wa Ramadhaan ilihali sio tena wasafiri. Kwa hivyo wanalazimika wawili hao kulipa siku hiyo na kutoa kafara. Wanapaswa kulipa siku hiyo ambayo kumetokea jimaa na kafara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22870/حكم-من-جامع-في-رمضان-بعد-عودة-من-سفر
  • Imechapishwa: 05/09/2023