09. Ni lini Mtume alisafiri na ami yake kueleka Shaam?

Swali 9: Ni lini alisafiri (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ami yake kueleka Shaam?

Jibu: Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na umri wa miaka kumi na miwili. Katika mwaka huohuo ndio mtawa Bahiyraa alimuona na alama zinazoashiria unabii wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamwamrisha ami yake kumrudisha nyumbani.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 93
  • Imechapishwa: 05/09/2023