Katika hali hizi tatu jihaad inatangulizwa mbele ya kila kitu

Swali: Jihaad ikiwa ni faradhi kwa kila mmoja inatangulizwa mbele ya kuwatendea wema wazazi?

Jibu: Jihaad ikiwa ni faradhi kwa kila mmoja basi inatangulizwa mbele ya kila kitu. Kwa mfano adui amevamia mji, akawa kati ya safu mbili au akateuliwa na kiongozi. Jihaad inakuwa ni faradhi kwa kila mmoja katika hali hizi tatu:

1 – Adui anapovamia mji. Ni wajibu kwa kila mmoja kutetea mji kwa kiasi cha uwezo.

2 – Kiongozi anapomteua mtu. Italazimika kwa mtu huyo kupambana.

3 – Anapohudhuria safu mbili. Asigeuze mgongo na kukimbia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22865/هل-يقدم-الجهاد-المفروض-على-بر-الوالدين
  • Imechapishwa: 05/09/2023