Je, inafaa kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa?

Swali: Je, inafaa kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa?

Jibu: Ni Sunnah. Ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa.

Swali: Baada ya swalah za faradhi au baada ya swalah zinazopendeza?

Jibu: Katika kila wakati. Isipokuwa katika yale maeneo ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono yake. Mfano wa maeneo hayo ni baada ya swalah za faradhi; hakunyanyuliwi mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono. Mfano wa maeneo mengine ambayo hakunyanyuliwi mikono ni katika Khutbah ya ijumaa na Khutbah ya ´iyd.  Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba du´aa katika Khutbah ya ijumaa na Khutbah ya ´iyd bila ya kunyanyua mikono yake. Lakini akiomba du´aa ya kuomba kunyesheleza katika Khutbah ya ijumaa, swalah ya kuomba manyeshelezo au maeneo mengine anyanyue mikono yake. Akiomba kuteremshwa mvua aombe msaada kutoka kwa Allaah na anyanyue mikono yake. Hivo ndio Sunnah. Watu pia watanyanyua mikono yao. Hukumu ni hiyohiyo wakati atapomba katika maeneo mengine. Akiomba nyumbani kwake, ndani ya gari yake, ndani ya ndege yake na mahali pa kuswalia atanyanyua mikono yake. Ni miongoni mwa sababu za kuitikiwa du´aa. Isipokuwa katika yale maeneo ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakunyanyua mikono yake. Akimaliza swalah ya faradhi asinyanyue mikono yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akinyanyua mikono yake baada ya kumaliza kuswali swalah ya faradhi; si Dhuhr, ´Aswr, Maghrib, ´Ishaa wala Fajr. Hakuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akinyanyua mikono katika swalah hizi. Vivyo hivyo kati ya Sujuud mbili wala mwishoni mwa swalah. Hakuwa akinyanyua mikono. Aombe du´aa bila ya kunyanyua mikono, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akinyanyua mikono.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23162/حكم-رفع-الكفين-اثناء-الدعاء
  • Imechapishwa: 26/11/2023