148. Yeyote anayejifananisha na watu basi ni katika wao

3 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nimetumilizwa kabla ya kusimama Saa kwa upanga mpaka aabudiwe Allaah hali ya kuwa ni Mmoja – asiyekuwa na mshirika. Riziki yangu imefanywa ni kutoka chini ya kivuli cha mkuki wangu, unyonge na udhalilifu umefanywa kwa yule anayeenda kinyume na amri yangu, na yeyote mwenye kujifananisha na watu basi huyo ni katika wao.”[1]

[1] Ahmad (5114, 5115 na 5667), al-Khatwiyb katika ”al-Faqiyh wal-Mutafaqqih” (2/73) na Ibn ´Asaakir (1/96) kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Thaabit bin Thawbaan: Hassaan bin ´Atwiyyah ametuhadithia, kutoka kwa Abu Muniyb al-Jarashiy, kutoka kwa Ibn ´Umar. Cheni ya wapokezi ni nzuri. Ni kweli kwamba Ibn Thawbaan ametajwa, lakini haidhuru. Sehemu ya Hadiyth imepokelewa na al-Bukhaariy, ingawa ni kwa cheni ya wapokezi pungufu. Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Ni utangulizi wa Hadiyth aliyoipokea Ahmad kupitia kwa Abu Muniyb… Inatiwa nguvu na njia nyingine inayokosa Swahabah katika cheni yake ya wapokezi. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri na ameipokea Ibn Abiy Shaybah, kupitia kwa al-Awzaa´iy, kutoka kwa Sa´iyd bin Jabalah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye ameitaja Hadiyth yote.” (Fath-ul-Baariy)

Kipande chake cha mwisho amekipokea Abu Daawuud, kupitia kwa Thaabit. Ibn Taymiyyah amesema:

”Cheni hii ya wapokezi ni nzuri.”  (Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiymm, uk. 39)

Haafidhw al-´Iraaqiy amesema:

”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.” (Takhriyj Ihyaa’ ´Uluum-id-Diyn (1/342))

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Cheni hii ya wapokezi ni nzuri.” (Fath-ul-Baariy (10/222)

Amesema vilevile kuwa imethibiti katika ”Fath-ul-Baariy” (10/274).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 203-204
  • Imechapishwa: 26/11/2023