Kwa njia inayolingana na Allaah

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) anasema: “Mimi niko vile mja Wangu anavyonidhania na Mimi ni pamoja Naye anaponitaja. Akinitaja kwenye nafsi yake Nami namtaja kwenye nafsi Yangu, akinitaja katika kundi, Nami namtaja katika kundi ambalo ni bora kuliko wao, akijikurubisha Kwangu paa moja Nami najikurubisha kwake dhiraa, akijikurubisha Kwangu dhiraa Nami najikurubisha kwake kwa kiasi cha kunyoosha mkono hadi kati ya kifuwa na akinijia kwa mwendo mdogo basi Mimi nitamjia kwa kuchapuka.”[1]

Je, inazingatiwa ni miongoni mwa Hadiyth za sifa za Allaah?

Jibu: Ndio, inapitishwa kwa udhahiri wake kwa njia inayolingana na Allaah. Ni miongoni mwa Hadiyth zinazozungumzia sifa za Allaah kwa njia inayolingana na Allaah.

[1] al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675) na al-Bukhaariy.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23174/معنى-الصفة-في-حديث-تقربت-اليه-باعا
  • Imechapishwa: 26/11/2023