I´tiqaad ya Ahl-us-Sunnah ni kupigana Jihaad nyuma ya watawala wa Kiislamu

Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tunaonelea Hajj na Jihaad inafanywa na viongozi wote, sawa akiwa ni mwema au muovu. Hali kadhalika inajuzu kuswali swalah ya ijumaa nyuma yao.”

Miongoni mwa sifa za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kwamba wanaonelea kuhiji na kupigana Jihaad litaendelea kuwepo pamoja na viongozi wa waislamu. Ni mamoja wakawa ni wema au waovu. Inahusiana na maimamu ambao:

a) Uongozi wao umepita kwa kuteuliwa na Ahl-ul-Hall wal-´Aqd[1].

b) Uongozi wao umepita kwa kutumia mabavu.

Uongozi wote huu unahesabika ni wa Kishari´ah. Wana haki ya kutiiwa katika mema na kupigana Jihaad nyuma yao na kutowaasi. Kuwatii wao ni kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuwafanyia uasi au kutoamini kwamba ni wajibu kuwatii ni I´tiqaad ya Khawaarj na Mu´tazilah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/ni-kina-nani-ahl-ul-hall-wal-aqd-wanaomteau-mtawala/

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 149
  • Imechapishwa: 27/08/2020