Swali: Ni kina nani Ahl-ul-Hall wal-´Aqd katika Uislamu? Je, upigaji kura unazingatiwa ni njia ya kuwateua?

Jibu: Ahl-ul-Hall wal-´Aqd ni wanachuoni wenye busara na watawala. Hawa ndio Ahl-ul-Hall wal-´Aqd ambao inatakiwa kuwarejelea na kuwauliza mambo yasiyokuwa na dalili. Hata hivyo haulizwi yeyote wakati maandiko ya Allaah yako wazi. Mfano wa wanachuoni hawa ambao sio Hizbiyyuun ni ndugu yetu Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab [al-Wusswaabiy], Abul-Hasan[1] na wanachuoni wengine wa Yemen wenye mfumo kama wao na ambao sio Hizbiyyuun. Kadhalika baadhi ya watawala wengine ambao wanataka kujikwamua na kila kinachoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/category/makala/manhaj/8-watu-wenye-makosa-makubwa-ambayo-wanachuoni-wametahadharisha/abul-hasan-mustwafaa-bin-ismaaiyl/

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=TqXGtSR1db4
  • Imechapishwa: 19/04/2015