I´tikaaf tarehe 21 baada ya Fajr

Swali: Mwenye kukaa I´tikaaf anaianza kuanzia Fajr ya tarehe ishirini au usiku wa tarehe ishirini?

Jibu: Aanze I´tikaaf Fajr ya tarehe ishirini na moja. Hapana vibaya akilala usiku huo hali ya kuwa ni mwenye kukaa I´tikaaf. Lakini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiingia I´tikaaf yake akishaswali Fajr.”

Bi maana kuanzia tarehe ishirini na moja.

Swali: Je, usiku wa Qadar si unakuwa usiku wa tarehe ishirini na moja?

Jibu: Ndio, unaweza kuwa tarehe 21 na 23. Unahamahama katika nyusiku zote kumi za Ramadhaan. Iliwahi kutokea usiku wa Qadar ukaangukia tarehe ishirini na moja katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Swali: Kwa hiyo mwenye kukaa I´tikaaf anaingia baada ya Fajr?

Jibu: Ataswali pamoja na waislamu msikitini hata kama hajaanza kukaa I´tikaaf.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22333/متى-يبدا-وقت-الاعتكاف-في-رمضان
  • Imechapishwa: 10/02/2023