Ibn Baaz kuhusu ´Umrah katika Rajab

Swali: Umetaja kwamba kufanya ´Umrah katika Rajab inapendeza kutokana na Hadiyth ya Ibn ´Umar. Ni katika kitabu gani tunaweza kuyarejelea hayo?

Jibu: Hadiyth ya Ibn ´Umar iko kwa al-Bukhaariy na Muslim. Hata hivyo ´Aaishah alimkemea na akasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya ´Umrah ndani ya Rajab. Mtunzi wa ”al-Latwaaif” ametaja Hadiyth ya Ibn ´Umar na ametaja kuwa ´Umar alikuwa akifanya ´Umrah katika Rajab na ametaja kutoka kwa Muhammad bin Siyriyn kutoka kwa Salaf kwamba walikuwa wakifanya ´Umrah katika Rajab. Kwa hiyo hapana neno na vibaya kufanya ´Umrah katika Rajab.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22334/هل-صح-شيء-في-العمرة-بشهر-رجب
  • Imechapishwa: 10/02/2023