Nchi ya kikafiri kwa ajili ya biashara

Swali: Vijana wanasafiri kutokea Ufaransa kwenda katika nchi ambayo kuna madhambi kwa ajili ya biashara. Je, ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika mimi nimejitenga mbali na kila muislamu anayeishi kati ya washirikina. Mioto yao haitakiwi kukaribiana.”

Kwa hiyo haijuzu kusafiri kwenda katika miji ya washirikina. Lakini hapana vibaya akiwa anaishi katika nchi na akawa anaijua dini yake, ana elimu na utambuzi na pia anadhihirisha dini yake. Ama akiwa ni mjinga haijuzu kwake kusafiri kwenda katika miji ya washirikina wala kuishi katika nchi zao. Bali ni lazima kwake kuhajiri kwenda katika nchi ambayo ana usalama juu ya dini yake. Asende kufanya biashara katika miji ya washirikina.

Swali: Akatazwe?

Jibu: Ndio, akatazwe. Isipokuwa kama yuko na elimu ambapo atalingania kwa Allaah na kuwafunza watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22330/حكم-السفر-لبلدان-الكفر-والمعاصي-للتجارة
  • Imechapishwa: 10/02/2023