Swali: Iqaamah za Oman ni mfano wa adhaana.

Jibu: Haya yamepokelewa katika baadhi ya Hadiyth ikiwa ni pamoja na Hadiyth ya Abu Mahdhuurah. Hapana vibaya kufanya hivo. Lakini kufanya Itaarah ndio bora zaidi kama ambavo Bilaal alivokuwa akifanya mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Maana yake ni kwamba asikariri “ash-Hadu anlaa ilaaha illa Allaah” wala “Haiyyaa ´alaa as-Swalaah”. Bali kila kimoja katika hayo akilete mara moja. Akiyakariri hapana neno kutokana na Hadiyth ya Abu Mahdhuurah iliyoashiriwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/366)
  • Imechapishwa: 24/09/2021