Swali: Ikiwa tuko kazini na kuna umbali mfupi kutoka msikitini – je, tuadhini?

Jibu: Ni lazima kwenu kuswali msikitini pamoja na mkusanyiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”

Ikiwa mtazuiwa basi imewekwa katika Shari´ah juu yenu kutoa adhaana na kukimu maeneo yenu kutokana na ueneaji wa dalili za ki-Shari´ah juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/361)
  • Imechapishwa: 25/09/2021