Kuzungumza wakati wa swalah ya khofu

Swali: Je, imeharamishwa kuzungumza ndani ya swalah ya khofu kwa ambaye analinda?

Jibu: Ikiwa ni ndani ya swalah basi asizungumze isipokuwa kwa yale yanayohusiana na adui. Lakini akiwa nje ya swalah inafaa kwake kuzungumza. Kwa sababu swalah ya khofu ina mbalimbali. Wakati fulani kikosi kundi wanakuwa wamelinda na wamepiga Takbiyr nyuma ya imamu. Katika hali hii kusizungumzwe isipokuwa wakati wa haja. Ama akiwa ni mwenye kulinda na hajaingia ndani ya swalah inafaa kwake kuzungumza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 24/09/2021