Swalah ya ´iyd ikiangukia siku ya ijumaa

Swali: Je, kuswaliwe ijumaa endapo siku ya ´iyd itaafikiana na siku ya ijumaa au itatosheleza kuswali swalah ya Dhuhr?

Jibu: Siku ya ijumaa ikiafikiana na siku ya ´iyd basi ijumaa itadondoka kwa yule aliyehudhuria ´iyd. Isipokuwa imamu haidondoki kutoka kwake. Swalah ya ijumaa itadondoka kwa ambaye amehudhuria ´iyd. Lakini ataiswali kama Dhuhr. Na ikiwa atahudhuria na akaswali ijumaa ndio bora. Kwa ambaye hakuhudhuria swalah ya ´iyd itamlazimu kuswali swalah ya ijumaa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (22)
  • Imechapishwa: 24/09/2021