Swali: Inajuzu kuwazika maiti usiku?

Jibu: Ndio. Inajuzu kuzika usiku maadamu mtu amefanya yale ya wajibu; maiti ameoshwa na amevikwa sanda na baada ya hapo ameswaliwa swalah ya jeneza. Katika hali hiyo inajuzu kuzika usiku. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizikwa usiku. Inasemekana vilevile kuwa Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) alizikwa usiku. Kadhalika mwanamke ambaye alikuwa akifuagia msikitini alizikwa usiku. Asli ni kujuzu. Kwa hiyo haya yanafahamisha kuwa kuzika usiku inajuzu kwa sharti kufanywe yale ya wajibu; kuoshwa, kuvikwa sanda na kuswaliwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/180)
  • Imechapishwa: 23/08/2021