Inajuzu kwa mlezi wa maiti kuwaomba wahudhuriaji kumsamehe yule maiti?

Swali: Inajuzu kwa mlezi wa maiti kuwaomba wahudhuriaji kumsamehe yule maiti?

Jibu: Mlezi wa maiti kuwaomba wahudhuriaji wamsamehe yule maiti ni Bid´ah. Sio katika Sunnah kuwaambia wale wahudhuriaji “Msameheni”. Midhali hana lolote na wao, basi hawana nyoyoni mwao kitu. Ikiwa alikuwa na chochote baina yake na wao na akafanya lile ambalo ni wajibu kwake kufanya juu ya yule mwingine, moyoni mwa yule mwingine hakuna kitu. Ikiwa hakufanya lile linalomlazimu juu ya yule mwingine, huenda akamsamehe na huenda asimsamehe. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuchukua mali ya watu kwa nia ya kutaka kuilipa, basi Allaah atamlipia nayo. Na yule mwenye kuchukua mali ya watu kwa njia ya kutaka kuiharibu, basi Allaah atamuharibia nayo.”[1]

[1] al-Bukhaariy (2387).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/216)
  • Imechapishwa: 23/08/2021