Ni Sunnah kuweka vichaka vya kijani na kitu kingine kwenye kaburi?

Swali: Je, ni Sunnah kuweka vichaka vya kijani au kitu kingine kwenye kaburi kwa kutumia dalili ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo kwa wale watu wawili wanaoadhibiwa ndani ya makaburi yao au hilo ni jambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kuweka tawi/mti wa kijani au kitu kingine kwenye kaburi sio Sunnah. Ni Bid´ah na ni kuwa na dhana mbaya kwa yule maiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa akifanya hivo kwa makaburi yote. Alifanya hivo kwa yale makaburi mawili kwa kuwa alijua kuwa ni wenye kuadhibiwa. Kuweka kuti kwenye kaburi lake ni tendo kubwa la jinai na kuwa na dhana mbaya kwake. Haijuzu kwa yeyote kumjengea dhana mbaya nduguye muislamu. Yule mwenye kuweka kuti kwenye kaburi la mtu ni kwamba anaonelea kuwa anaadhibiwa, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya hivo pale alipojua kuwa wale wawili ni wenye kuadhibiwa. Kwa kufupisha ni kwamba kuweka kuti au kitu kingine kwenye kaburi ni Bid´ah isiyokuwa na asli. Aidha ni kumjengea dhana mbaya yule maiti kwa kuwa anafanya hivo kwa sababu anaonelea kuwa anaadhibiwa na hivyo ndio maana anatakiwa kumkhafifishia. Jengine ni kwamba hatujui kuwa Allaah anaitikia uombezi wetu juu ya yule maiti endapo tutafanya hivo. Vilevile hatujui kabisa kama yule aliyemo ndani ya kaburi anaadhibiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/191-192)
  • Imechapishwa: 23/08/2021