Imewekwa katika Shari´ah kumfunika maiti kwa kitambaa kilicho na Aayah za Qur-aan?

Swali: Katika baadhi ya sehemu wanamfunika maiti kwa kitambaa kilicho na Aayah al-Kursiy au Aayah za Qur-aan. Je, kitendo hichi kina asli?

Jibu: Kitendo hichi hakina asli. Bali uhakika wa mambo ni kuyatweza maneno ya Allaah (´Azza wa Jall) kwa kuyafanya ni kitambaa anachofunikiwa maiti. Hayamnufaishi maiti kitu. Kwa ajili hiyo ni wajibu kuliepuka. Mosi sio katika matendo ya Salaf. Pili ni kuitweza Qur-aan tukufu. Tatu kitendo hichi kina I´tiqaad mbovu ambapo mtu anafikiria kuwa kitambaa hiki kinamnufaisha maiti, jambo ambalo si kweli.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/168)
  • Imechapishwa: 23/08/2021