Kusimama pembezoni mwa kaburi na kumwangalia maiti imewekwa katika Shari´ah?

Swali: Baada ya maiti kuwekwa ndani ya kaburi watu wengi wanalizunguka kaburi na kumwangalia yule maiti. Je, kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Hakikuwekwa katika Shari´ah. Kilichowekwa katika Shari´ah pindi maiti anapowekwa ndani ya kaburi ni kumfunika kwa kokoto halafu kumzika moja kwa moja. Kilicho bora ni kufanya haraka katika kuzika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/180)
  • Imechapishwa: 23/08/2021