Inajuzu kuwafanyia ghushi Ahl-ul-Bid´ah na makafiri?

Swali: Ghushi ni haramu. Je, inajuzu kuwafanyia ghushi mapote potevu na makafiri?

Jibu: Hapana. Haijuzu kumfanyia kumdhulumu yeyote, hata adui:

وَلَا يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَىٰ أَلَّا تَعْدِلُوا ۚ اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَىٰ ۖوَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ

“Na wala chuki ya watu isikuchocheeni kutokufanya uadilifu. Fanyeni uadilifu, hivyo ni karibu zaidi na taqwa. Na mcheni Allaah; hakika Allaah mjuzi kwa myatendayo.” (05:08)

Haijuzu kumfanyia ghushi yeyote wala kumdhulumu yeyote. Ni wajibu kufanya uadilifu hata ikiwa ni kwa adui:

اعْدِلُوا هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى

“Fanyeni uadilifu; hivyo ni karibu zaidi na taqwa.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (09) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340324.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2015