Swali: Khawaarij ni wale wanaofanya uasi kwa kiongozi ambaye ni muadilifu tu. Ama yule mwenye kufanya uasi kwa kiongozi dhalimu sio katika Khawaarij.

Jibu: ´Abdul-Maalik alikuwa ni kiongozi dhalimu na alifikia mpaka kumuua ´Abdullaah bin az-Zubayr na akaamriaha kubomoa Ka´bah. Pamoja na yote haya ´Abdullaah bin ´Umar na Maswahabah waliokuwepo wakampa bay´ah. Kwa kweli alikuwa ni dhalimu. Allaah Amrahamu. Alikuwa na mazuri na mema yake, lakini hata hivyo alikuwa ni dhalimu na mkandamizaji. Tazama msimamo wa Maswahabah ulivokuwa mbele yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifundisha na maandiko yanapatikana katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na ya Muslim na katika vitabu vinginevyo:

“Watiini maadamu wanaswali.”

“Mtaona mambo mnayoyajua na mnayoyapinga.”

Wakasema: “Je, tusiwapige vita?”

Akajibu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hapana, midhali wanaswali.”

Ni watawala madhalimu lakini pamoja na haya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaamrisha kuwa na subira juu yao na kwamba haijuzu kuwafanyia uasi. Mwenye kutela mfarakano katika umoja wa Waislamu ni wajibu kumuua hata kama atamfanyia kiongozi ambaye ni dhalimu. Hizi ni fikira za ki-Khawaarij.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliybin Haadiy al-Madkhaliy ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=26877
  • Imechapishwa: 19/05/2015