Swali: Tunajua kuwa kuwasengenya Ahl-ul-Bid´ah inajuzu. Lakini je, hilo lina masharti? Ikiwa jibu ni ndio, ni zipi sharti hizo?

Jibu: Kuwasengenya Ahl-ul-Bid´ah, au kwa msemo mwingine kutahadharisha nao na kuwanasihi watu wasidanganyike nao ni wajibu na ni katika Jihaad kubwa. Si kwamba inajuzu tu, bali ni wajibu. Wakati unapowaona watu wanakimbilia katika fitina na wanatumbukia katika Bid´ah na upotevu halafu unanyamaza na kusema ni kusengenya! Huku ni kufanya khiyana na ghushi. Wewe unawaona watu wanatumbukia katika fitina kama jinsi magodoro yanavyotumbukia ndani ya moto na wewe huku umenyamaza. Mashaa Allaah mnyenyekevu! Huu ni unyenyekevu wa uongo. Huu ni unyenyekevu wa wajinga na wapotevu katika Suufiyyah waliopotoka na watu mfano wao na walioathirika na wao. Kusema haki ni wajibu:

فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ

“Basi tangaza wazi yale uliyoamrishwa na jitenge na washirikina.” (51:94)

Wakengeuke washirikina na watu wa Bid´ah na walio mabubu katika haki na kupambana na batili. Kuna masharti mawili:

1- Umtakasie nia Allaah na ukusudie kwa hilo ujira kutoka kwa Allaah.

2- Ukusudie kuwapa nasaha Waislamu na kuwalinda na shari.

Ni lazima kupatikane masharti haya mawili.

Ama kumzungumzia huyu na yule – hata kama atakuwa ni kafiri – kwa sababu ya mambo ya kibinafsi, hii sio katika nasaha iliyowekwa. Bali ni katika tabia mbaya ambayo mtu anapata madhambi kwayo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: adh-Dhariy´ah ilaa Bayaan Maqaasid Kitaab-ish-Sharï´ah (1/204)
  • Imechapishwa: 19/05/2015